CCM Yamuonya Polepole "Awe na Nidhamu na Adabu Kama Aliyokuwa Nayo Awamu ya 5"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




KATIBU Mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kenani Laban Kihongosi amesema wanasikitishwa na matendo yanayofanywa na Mbunge Humprey Polepole kuhusu suala la chanjo, kwani Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshasema Kwamba chanjo ni hiari na maamuzi yake lazima yaheshimiwe.


“Tunapenda kumwambia Mbunge Polepole kwamba awe na nidhamu na adabu kama aliyokuwa nayo wakati wa Utawala wa Awamu ya Tano, nidhamu ileile aiendeleze pia katika Utawala huu wa Awamu ya Sita Inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, mijadala yake kuhusu chanjo ni bora akakaa kimya kama haitaji kuchanjwa, lakini sio kujificha katika kivuli cha chanjo kuipinga Serikali.


“Kamwe hatutovumilia utovu wowote wa nidhamu kwa Rais Samia na Serikali yake, sasa kuendelea kutengeneza maneno ya kejeli, dhihaka na mengine ya aina hiyo yanabeba mazingira yanayotia shaka dhamira yake aliyonayo kwa Mwenyekiti wetu na Rais wetu wa Tanzania, tunamtaka aache mara moja.

“Chama cha Mapinduzi sio Chama cha harakati bali ni Chama kilichojijenga katika misingi ya kutii na kuheshimu Viongozi, hivyo jambo lolote la kupinga au kuendeleza mijadala ambayo Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshaitolea maelekezo ni utovu wa nidhamu kwa Chama na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.

“Tunamuonya na tunamtaka aache mara moja kwani hatutakubali Kiongozi yoyote avunje heshima ya Rais Samia Suluhu Hassan au kupinga yale aliyoyaelekeza,” amesema Kihongosi.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad