.

8/23/2021

Chanzo Cha Ajali Wafanyakazi wa TRA Cha Tajwa...Kumbe Walikuwa Wanafukuza Gari Lingine
Watumishi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki kwa ajali katika eneo la Hanseketwa – Old Vwawa wakati wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo.


Ajali hiyo imetokea baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya Toyota Land Cruiser kugongwa kwa nyuma na lori la mizigo aina ya Fuso leo Agosti 23, 2021 majira ya saa 11 alfajiri katika eneo hilo la Hanseketwa wilayani Mbozi, Songwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Taarifa Zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger