.

8/19/2021

Chemical Amjibu Rosa Ree Kuhusu Kufanya Ngoma Pamoja.. "Mimi Binafsi Sina Chuki Na Msanii Yoyote"


Baada Ya Siku Ya Jana @rosa_ree Kuonesha Nia Ya Kufanya Kazi Na Female Rappers Wenzie @fridaamaniofficial Pamoja Na @chemical_tz Ambayo Huenda Project Hiyo Ikawa Kwenye Album Yake Ambayo Anatarajia Kuitoa Soon, Rapper @chemical_tz Ameonesha Kupendezwa Na Kitu Hicho Na Kusema Yupo Tayari Kolabo Hiyo Na Kufunguka Kuwa Pia Ni Kitu Kizuri Maana Wasanii Wakike Ni Wachache Kwenye Game Hivyo Kushirikishana Kama Hivyo Ni Kitu Kikubwa.

Kupitia Zege Ya Times Fm Chemical Amesema “Ni Kitu Kizuri Sana, Lakini Ni Kama Matamanio Tu Bado Hakijafanyika Ni Kwamba Yeye Ametamani Mimi Niwepo Kwenye Album Yake Na Mimi Nakichukulia Kwa Uchanya Zaidi, Wasanii Wakike Kwenye Game Wapo Wachache Sana Kwahiyo Ukiona Msanii Mwenzio Wakike Anataka Kukushirikisha Basi Ujue Ni Kitu Kikubwa Sana, Hivi Ikitokea Imefanyika Nitafurahi Na Isipo Fanyika Pia Watu Wajue Haikuwezekana Tu, Mimi Binafsi Sina Chuki Na Msanii Yoyote”

Kwa Habari Zaidi, Usiache Kutembelea Youtube Channel Yetu Ya Swahili Media
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger