.

8/18/2021

Danie Craig (James Bond) Adai Akifa Watoto Wake Wasipe Urithi Wowote, Kisa na Mkasa Huu Hapaa


Miongoni mwa waigizaji wenye mafanikio kwenye tasnia ya filamu ni Danie Craig (James Bond), hivi karibuni amefunguka kwamba hatowaachia watoto wake utajiri wa pesa zake pindi akiondoka duniani. Daniel Craig amepanga kuzitumbua zote mpaka umauti unamkuta.

Muigizaji huyo ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa ($160 million) zaidi ya TZS. Bilioni 371 akiwa ana watoto wawili wa Kike, amesema suala la urithi ni dhana ambayo haina mashiko kwani anaamini kwenye kutoa na kutumia mali yako kabla hujaondoka duniani.

"Nafikiri urithi ni dhana isiyo na mashiko. Falsafa yangu ni kuzitumia au kutoa kwa njia ya misaada kabla hujaondoka duniani. Alisema Daniel Craig ambaye anaungana na mastaa wengine kama Jackie Chan, Gordan Ramsey, Sting na Simon Cowell ambapo wametangaza kutowaachia urithi watoto wao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger