.

8/01/2021

Davido Amfukuza Kazi Meneja Wake Kisa Tapeli Tapeli Hush Pupi
Wiki hii imekuwa na pilikapilika nyingi mahakamani huko nchini Marekani katika kuendesha kesi za wahalifu wa mitandaoni mmoja wapo akiwa ni Mnigeria @hushpuppi ambaye amekiri kufanya makosa ya kimtandao ikiwemo kuhack account zenye mitonyo kibao na kujipatia pesa hisivyo kihalali.

Kukiri makosa kumefanya Mahakama kumtwanga mvua ya miaka 20 jela tajiri Hush Puppi ambaye aliwekwa kizuizini toka mwaka jana,July 2020 hadi wiki hii alivyo hukumiwa kwenda Lupango.

Ishu hii imemfanya msaidizi na meneja wa Davido kwenye masuala ya safari na usafirishaji bwana @isrealdmw atoe maoni akimlaumu Davido kutofanya jitihada zozote kumsaidia mshikaji wake Hush Puppi ambaye amekula nae good time mara nyingi sana akiwa uraiani.

Kitendo hiki kimemuudhi msanii Davido na kumsimamisha kazi jamaa huyo kwa muda usiojulikana lakini pia Davido kaamua kumuunfollow kabisa kwenye mtandao wa Instagram kuonyesha kuchukizwa na maoni yake.

Usiache kufollow Sajomedia kwa taarifa mbalimbali za burudani.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger