.

8/15/2021

DC Msando Ahamishiwa Muhimbili Kwa Uchunguzi zaidi Baada ya AjaliWatu watano wamejeruhiwa katika akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando na Mkuu wa Wailaya ya Ulanga, Ngollo Malenya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutokea Mbigiri – Dakawa Wilaya ya Kilosa kuelekea Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Toyota Land Cruser yenye namba za usajili DFPA 8530 iliyokua ikitokea Morogoro Mjini kueleke Dodoma .


Kaimu Mganga mfawidhi hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro, Dk. Kessy Ngallawa amethibitisha kupokea majeruhiwa hao majira ya saa 7 mchana leo Agosti 14 akiwemo wakuu hao wa wilaya, Dereva wa gari ya mkuu Wilaya Morogoro na wauguzi wawili walikua kwenye gari iliyopata ajali

Hata hivyo mganga huyo amesema baada ya kupata matibabu ya awali wakuu wa wilaya wamehamishiwa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibababu.

Kwa upande wake dereva wa gari wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Morogoro iliyopata ajali Mohamedi Juma ambaye ni miongoni mwa majeruhi amesema walikua wanawahi msafara wa waziri mkuu uliokua ukitokea Mbigiri kuelekea mjini Morogoro.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger