.

8/27/2021

Diamond Platnumz Atahamia Yanga Kumfuata Haji Manara?Msanii Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa alianza kushabikia mpira na kuishabikia timu ya Simba mara baada ya kupata hamasa kutoka kwa swahiba wake Haji Manara.

Kama hiyo haitoshi ,Diamond alilaani sana kipindi ambacho mabosi wa Simba walipoanza kumtolea maneno machafu Haji Manara na alipoonesha yupo upande wa Haji viongozi wa Simba walimfungia vioo na kumblock kabisa Diamond huko kwenye kurasa zao za Instagram.

Sasa je, Diamond ataendelea kuishabikia Simba au atamfuata swahiba wake Haji kuja timu ya Wananchi Dar Es Salaam Young Africans??

Bila shaka Diamond akihamia Yanga, yule chawa Dulla Makabila bila shaka na yeye atarudi Yanga maana alihama Yanga kwenda Simba kumfuata Diamond Platnumz.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger