.

8/02/2021

Domokaya Amjibu Linex Kushuka kwa MuzikiDigala Domokaya ameijibu comment ya msanii Linex baada ya kutoa ujumbe unaosema kwamba muziki wa sasa Tanzania umeshuka hivyo wasanii wazuri wafanye jitihada za kuuridisha muziki.

Domokaya amesema muziki wa sasa hivi ni biashara na watu wamewekeza pesa zao hivyo hawataki kupata hasara ndio maana inatumika njia zote ku-push aina ya miziki hiyo.

"Sasa hivi muziki ni biashara watu wanatia pesa zao, kwa hiyo hawawezi kuweka pesa halafu wakapata hasara hivyo watapush kwa style yoyote hata kama hupendi, zingekuwa zinapata nafasi kazi nzuri na zenye ubora hata kama wasingeweka pesa ingehitajika sapoti tu na mziki mzuri wenyewe utajitangaza" amesema Domokaya

Kupitia comment hiyo aliyoitoa Linex kuhusu kushuka kwa muziki wa Bongo umezua mjadala kwa baadhi ya mashabiki, wasanii na wadau wa muziki mitandaoni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger