.

8/22/2021

Duniani Kuna Watu Hamnazo.. Mchungaji Aliyedai Azikwe Akiwa Hai Kuwa Atafufuka Akutwa Amekufa
Mchungaji wa kanisa la Zion nchini Zambia James Sakara (22), aliyewaomba baadhi ya waumini wake wamchimbie kaburi na kisha wamzike akiwa hai kwa madai ya kwamba baada ya siku tatu angefufuka kama Yesu, amekutwa akiwa amefariki dunia.

Mtu akichimba kaburi
Awali kabla ya maamuzi ya kuzikwa akiwa hai, baaadhi ya waumini wake walimkataza kufanya ujinga huo lakini baadaye, walijitokeza waumini wake watatu ambao waliamini madai yake ya kwamba angefufuka na kuamua kumzika na kwamba kabla ya kuzikwa aliwaambia waumini wake maneno haya.

"Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi," alisema mchungaji huyo.

Imeelezwa kuwa mara baada ya kumkuta amefariki dunia, waumini hao walianza kumfanyia maombi ya kumfufua tena jambo ambalo halikuwezekana.

Hadi sasa Jeshi la Polisi nchini humo linaendelea kuwashikilia waumini waliomsaidia kumzika akiwa hai mchungaji huyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger