.

8/19/2021

Gari Lamponza Nandy, Apewa Makavu Insta!

SHOO inaanza kwa mwalimu wa hesabu wa masanii Nandy kusakwa kwa kutotimiza wajibu wake wa kumfundisha mwanafunzi wake akaelewa.

 

Imekuwaje Wananzego wakafikia huko? Ni kitendo cha msanii huyo kudaiwa kuwatia changa la macho  watu kwa kuwaamba uongo kwamba, thamani ya gari lake jipya ni matumizi ya laki moja kwa miaka 60.


Nandy alihojiwa hivi karibuni na wapekuzi wa habari fulani ambao walitaka kujua gari lake jipya
alilonunua kama angeweka shilingi laki moja kila siku ingemchukua miaka mingapi kuweza kulinunua?

 

Yeye bila woga akajibu “Ingenichukua miaka sitini kuweza kufikia thamani ya gari hilo.”Unajua gari lenyewe ni aina gani ambalo msanii huyo amenunua baada ya kulamba dili la ubalozi fulani hivi?Ni Ranger Rover Evoque ambalo watu wanadai halizidi hata shilingi milioni 80. Zile kejeli za gari lenyewe ni la mtumba ziweke kando.Kimbembe cha kutojua hesabu; kikamwangukia Nandy, amekula michambo mitandaoni ile mbaya na kuambiwa kabisa “kichwani hesabu ni ziro.”


“Huyu ana tatizo kubwa, sijui amepatwa na nini; Evoque ni kama milioni 75 tu, laki kila siku unatimiza kwa siku 900 tu ambayo ni sawa na miaka miwili kama na nusu hivi, sasa hiyo miaka 60 inakujaje?” Mtu mmoja
alihoji mtandaoni.

 

Mwingine aliandika: “Ina maana hata gari la Diamond RR liko chini kwa thamani; miaka 60 ukijiwekea laki kila siku unapata kama Bilioni 2 na zaidi na gari la Diamond ni kama bilioni 1, hii ndiyo Bongo ya wasanii waliokubuhu kwa uongo.”Kuna mmoja alijaribu kupoza mambo kwa kusema: “Msameheni kaongeza zero kwa bahati mbaya.”

 

Mwingine alipokuja yeye alitumia lugha ya matusi, yaani ni kama gari limemponza Nandy na kujikuta
akitukanwa na Wananzengo wenye chuki na maendeleo ya watu.

 

Lakini mwisho wa siku jamani Nandy awe amekosea hesabu, awe hajui hesabu, muongo ilimradi gari kanunua basi apewe heshima yake mjini na kupongezwa au vipi?


Maana bila shaka, tena kwa uhakika kabisa Nandy ni miongoni mwa wasanii wachache wa kike wanaopambana kwa jasho na damu kufikia ndoto zake za maisha kwa kutumia kipaji chake cha muziki


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger