.

8/18/2021

Habari Mbaya: Wafanyakazi wa Ayo TV Wapata Ajali, Wawili Wafariki

TAARIFA iliyotufikia hivi punde ni kwamba wafanyakazi wawili wa Ayo TV mkoani Mwanza, wanaofahamika kwa majina ya Dullah TZA na Nelson Brigeri ‘Nelly TZA’ pamoja na mwenzao mmoja (ambaye si mfanyakazi wa Ayo TV) aliyefahamika kwa jina la Mujitaba Abbas wamepata ajali maeneo ya Kibaha usiku wa kuamkia leo Jumatano, Agosti 18, 2021 wakati wakiwa safarini kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.


Taarifa zinaeleza kuwa ndani ya gari hilo dogo binafsi kulikua na watu watatu ambapo mmoja wao, Nelly amepoteza maisha pamoja na Mujitaba naye amefariki dunia.
Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Ayo TV, Dar es Salaam, miili ya marehemu imeifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani ambapo pia Dullah aliyepata majeraha anaendelea na matibabu.
Nelly enzi za uhai wake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger