.

8/30/2021

Haji Manara Apata Ajali

Msemaji wa Yanga Haji Manara amekiri kupata ajali ‘mbaya’ ya gari jana usiku Jijini Dar es salaam na kusema alinusurika kwenye ajali hiyo ambayo imeliacha gari lake likiwa limeharibika vibaya.

Haji ameyasema hayo wakati akieleza sababu zilizomfanya ashindwe kufika kwenye mahojiano na kituo cha Radio cha Efm leo asubuhi ambapo ameandika “Usiku wa jana nilinusurika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kuharibika vibaya, hadi kuja kulala ilikuwa ni mida mibaya ya usiku mkubwa”

 

Alichokiandika Haji Manara.

Ndugu zangu EFM nawaomba radhi sana kwa kutofika kwenye kipindi asubuhi ya leo kama nilivyoahidi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu!!

 

Usiku wa jana nilinusirika na ajali mbaya ya gari baada ya gari yangu kugongwa vibaya na kusababisha kuharibika vibaya gari yangu. Hadi kuja kulala ilikuwa ni mida mibaya ya usiku mkubwa na sikuweza kuamka mapema ili niwahi kipindi chenu alfajiri ya leo saa kumi na Mbili.

 

Nawaomba tena radhi nyie na Wasikilizaji na watazamaji wote. Mnisamehe sana na nimejisikia vibaya sana. ๐Ÿ™๐Ÿ™


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger