.

8/15/2021

Harmo; Visasi Siyo Sehemu ya Maisha

KONDE Boy Mjeshi kunako Bongo Flevani, Rajabu Abdul au Harmonize anasema kuwa, kulipa visasi kwa maadui zake siyo sehemu ya maisha yake kwa sababu amelelewa kwenye maadili mema ya kuishi na watu vizuri.

 

Akizungumza na IJUMAA SHOWBIZ, Harmonize au Harmo anasema kuwa, mashabiki wake wengi huwa wanashangaa jinsi anavyowaposti watu aliokwazana nao, lakini hilo kwake ni jambo la kawaida na hufanya hivyo kwa nia njema ya kutaka amani.

 

“Nimelelewa kwenye maadili mazuri sana, sijafundishwa roho mbaya kabisa na ndiyo maana nina nidhamu kwa watu wa rika zote kwa sababu mwisho wa siku, ukiendekeza chuki huwezi kujua ni nani atakufaa baadaye.

 

“Ndiyo maana nasema visasi siyo sehemu ya maisha yangu kwa sababu napenda kuishi kwa amani na watu wote,” anasema Harmo ambaye anatrendi namba moja kwenye YouTube na Ngoma ya Mang’dakiwe Remix akiwa na Dj Obza na Leon Lee.

KIMENUKA! DULLAH MBABE AMKIMBIA TWAHA KIDUKU KWENYE FACE OFF “Hata UKIOGOPA, KICHAPO KIKO PALEPALE”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger