.

8/09/2021

Hatimaye Mchezaji Mohamed Hussein Afunguka "Mimi Ndio Mwenye MKE, Mimi Ndio Niliooa"

 


Mchezaji wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein aka Zimbwe, anataka watu wajue kuwa hajali kile walichosema kuhusu muonekano wa mke wake. Mohamed alifunga ndoa mwishoni mwa wiki na mtandaoni ikasambaa picha iliyochukuliwa vibaya ikimuonesha mkewe kama mtu mwenye umri mkubwa.

Kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Jumatatu hii, mchezaji huyo amesema ni mkewe ni mwanamke wa ndoto yake.

“Mimi ndio mwenye mke, na mimi ndio niliooa, uzuri wa mke wangu naufahamu mimi, na hakuna mtu yoyote anaweza akaja mbele akasema mke wangu ni mtu wa aina gani,” amesema Mohamed.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger