.

8/26/2021

Ibrah Ataja Sababu Za Kumposti Mke Wa Rayvanny


MKALI wa mkwaju wa Jipinde kutoka Lebo ya Konde Gang, Ibrah amesema kuwa alimposti mzazi mwenza na mpenzi wa zamani wa staa wa WCB, Rayvany, Fahyma kwa kuwa kwake ni kama dada.

Ibrah alisema kuwa, utofauti wake na Rayvanny hauwezi kumzuia yeye kuwaposti watu anaowapenda na alifanya hivyo siyo kwa ubaya bali ni kwa mapenzi yake mema kwa wanawake wa Kitanzania.
“Nilimposti Fahyma kwa sababu ni dada na mwanamke ambaye namkubali, haikuwa vile kwa sababu ya kumuumiza Rayvanny kwa sababu pengine tunatofautiana, haikuwa hivyo,” alisema Ibrah.

Ibrah na Rayvanny waliingia kwenye ‘kamgogoro’ kadogo baada ya Ibrah kumuimba Rayvanny kufuatia kukorofishana na Harmonize juu ya ishu ya mpenzi wake wa sasa, Paula.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger