.

8/12/2021

Imekuwa Vibaya Kwa Musiba..Aamriwa Kumlipa Fatma Karume Bil. 7.5/-MAHAKAMA Kuu Zanzibar imemwamuru Cyprian Musiba na Gazeti la Tanzanite, kumlipa fidia ya Sh. bilioni 7.5, Fatma Karume, baada ya kubaini alimchafua kwa kumzushia taarifa za uongo.

Uamuzi huo ulitolewa jana baada ya mahakama hiyo iliyoko Vuga kusikiliza madai ya Fatma dhidi ya Musiba na hoja za utetezi zilizowasilishwa na mlalamikiwa huyo.

Fatma aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea, alifungua kesi mwaka 2019 dhidi ya Musiba akilalamikia kuchafuliwa na mara ya kwanza ilitajwa Oktoba 3, 2019.

Katika madai yake, Fatma alimlalamikia Musiba kwa kumchafua kwa kumzushia taarifa za uongo zenye lengo la kushusha hadhi yake katika jamii.

Fatma anadai katika malalamiko yake kwamba, Musiba alimwambia ametiwa mimba na muuza unga na kwamba hana staha wakati anadai maelezo hayo si kweli kwa kuwa ana mume na watoto.


Katika kesi hiyo, Fatma alikuwa akiwakilishwa na Wakili Karume Mrisho ambaye alidai jana, kuwa mteja wake kwa sasa yuko nje ya nchi
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger