Jerry Silaa ataja sababu 3 kuikacha kamati ya Bunge

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga
MBUNGE wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ametaja sababu tatu, ikiwemo kwenda kwenye mazishi jijini Arusha na kutokuwa sawa kiafya, zilizomfanya jana Alhamisi, tarehe 26 Agosti 2021, asifike mbele ye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuendelea na mahojiano dhidi ya tuhuma zinazomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Silaa ametaja sababu hizo leo Ijumaa, tarehe 27 Agosti 2021, akizungumza na wanahabari, alipofika katika ukumbi wa Bunge, jijini Dodoma kwa ajili ya kuendelea na mahojiano baada ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, jana kumuomba Spika wa Bunge, Job Ndugai, atoe kibali kwa Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha mbunge huyo mbele ya kamati kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa.

Mwakasaka alimuomba Spika Ndugai atoe kibali hicho, baada ya Silaa kutofika mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuendelea na mahojiano aliyoyaanza siku ya Jumanne, tarehe 24 Agosti 2021.

Silaa amesema, baada ya kuhojiwa Jumanne, alipata taarifa za msiba ambao hakutaja ni wa nani, lakini hakuieleza kamati hiyo.


 Hivyo, jana Jumatano alisafiri kuelekea Arusha kwa ajili ya kushiriki mazishi.

“Nilihojiwa na kamati Jumanne na nilimaliza utetezi wangu, niliijulisha kwamba nimefiwa siku hiyo asubuhi niliona kwa picha ninayoiona ningewaambia wasingenielewa.”

“Kwa hiyo jana nilianza safari kwenda kwenye maziko Arusha na mimi kama watu wengine nikayakuta kwenye vyombo vya habari sababu sikuona waranti ya Polisi nikaona nifike leo, nikafika saa nne kasoro dakika moja kwenye kamati,” amesema Silaa.


Mbunge huyo wa Ukonga amesema, baada ya kufika mbele ya kamati hiyo, ameieleza kwamba jana hakufika kuhojiwa kwa sababu alikuwa na matatizo ya kiafya, pia hakupata wito wa kufika kwenye mahojiano jana.

“Suala moja nilieleza kwa nini sikufika, nikaeleza sikupata samansi sababu samansi niliyoipata ilikuwa ya siku ya Jumanne saa saba mchana na kwa mujibu wa sheria ya niliwasilisha utetezi nikamaliza hivyo, hivyo kamati yenyewe itamaliza. Lakini niliwaeleza sababu zote tatu, kuumwa, kwenda kwenye msiba na sikupata taarifa,” amesema Silaa.

Alipoulizwa na wanahabari kama alipomaliza mahojiano Jumanne hakuelezwa kama anatakiwa kurudi tena Alhamisi, Silaa alijibu kwamba hakumbuki kama alipewa taarifa.

“Sina kumbukumbu kama walinieleza,” amesema Silaa.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad