.

8/21/2021

Jinsi watu wanavyopambana kuitoroka Taliban

"Rudini nyuma , rudini nyuma " alisikika mwanajeshi wa Uingereza kwenye umati uliokuwa mbele ya kiwanja chenye usalama ambapo wale wanaohamishwa na ubalozi wa Uingereza huchukuliwa kabla ya kuondoka kwenda nje.


Mbele yake, wengi walionesha hati zao za kusafiria za Uingereza hewani, wakitumaini kuruhusiwa kupita lakini kundi la walinzi wa Afghanistan waliobeba mipira walijaribu kuwarudisha nyuma.
Wengi katika umati walikuwa hawajaambiwa chochote kwamba watahamishwa, lakini walikuwa wanatafuta namna yoyote ya kutoka Afghanistan.Wengine, hata hivyo, walikuwa wamepokea barua pepe kutoka kwa ubalozi wakiambiwa wafike hapo na kusubiri kushughulikiwa kupata ndege ya kuondoka nayo.Ni pamoja na Helmand Khan, dereva wa Uber kutoka magharibi mwa London, ambaye alikuwa amewasili na watoto wake wadogo huko Afghanistan miezi michache iliyopita kutembelea jamaa."Kwa siku tatu za mwisho najaribu kuingia ndani," ananiambia akiwa amekata tamaa, na wanawe wawili wadogo kando yake.Pia hapa kuna Khalid, mkalimani wa zamani wa jeshi la Uingereza. Mkewe alijifungua mtoto wiki mbili tu zilizopita na anaogopa mtoto anaweza kufa katika matukio kama haya. "Nimekuwa hapa tangu asubuhi," anasema, "Wataliban walinipiga mgongoni nilipokuwa njiani."Kutembea kwa muda mfupi kuelekea mlango kuu wa kiwanja, Maelfu wamejitokeza, idadi kubwa bila matarajio halisi ya wanaohamishwa.Wanajeshi wa Uingereza wakati mwingine walifyatua risasi hewani kudhibiti umati.Njia pekee ya kuingia ndani ni kwa kushinikiza kupenya katikati ya umati wa watu, na kupunga hati zao, wakitumaini wataruhusiwa kupita.Hali hiyo inaonekana kuwa ya vurugu zaidi katika milango ya uwanja wa ndege iliyo na wanajeshi wa Marekani, wakati mbele ya mlango kuu wa uwanja wa ndege wa Taliban wamekuwa wakifyatua risasi hewani mara kwa mara na kuuzuia umati ambao unajaribu kuingia ndani."Mimi hushambuliwa kila wakati na maswali na Waafghanistan ambao wanajaribu kuingia kwenye kiwanja kinachodhibitiwa na Uingereza, na ambao wamepoteza kabisa la kufanya."Unaweza kunisaidia?" "Wataniacha niingie?" Wengi hujaribu kunionesha nyaraka ambazo wamekuja nazo, ikithibitisha kuwa walifanya kazi na vikosi vya kimataifa au balozi za kigeni.Msichana mmoja ananiambia alikuwa mchezaji wa mpira wa magongo wa kimataifa.Hajapata mawasiliano yoyote na ubalozi wa Uingereza, lakini anasema anahofia maisha yake.Taliban wanasisitiza wale wote wanaohusishwa na serikali wamepewa msamaha.Kundi linasema linakusudia kuanzisha serikali "ya umoja", lakini wengi hapa wana wasiwasi mkubwa kuhusu ya siku zijazo.Mahali pengine katika jiji, mambo yametulia sana ni kama ulimwengu wa tofauti.Maduka na migahawa imefunguliwa, ingawa kwenye soko la matunda na mboga mboga wananiambia bado kuna watu wachache sana nje na karibu na maeneo hayo.Mwanaume mmoja, akiuza bidhaa za mapambo, anasema kuna wanawake wachache haswa, ingawa sio kawaida kuwaona barabarani.Wakati huo huo Taliban wako kila mahali, wakifanya doria katika magari yaliyokamatwa kutoka kwa vikosi vya usalama vya Afghanistan.Wanasema wanadumisha uwepo ili kuzuia uporaji na machafuko, na wakazi wengine wanatuambia wanahisi salama zaidi, haswa kwa sababu wanamgambo hawafanyi mauaji ya kulengwa au milipuko ya bomu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger