.

8/11/2021

Kanye West Anaendelea Kuwapiga Watu Hela..Kufanya Onyesho Katika Uwanja Mwingine


Huwenda tarehe 15 mashabiki wasiipate album mpya ya Kanye West #DONDA bali wajipange kwenda uwanjani tena kushuhudia uzinduzi wa album hiyo. Jana Jumatatu rapa Kaycyy ambaye anafanya kazi kwa ukaribu na Kanye kwenye project hii ya DONDA, aliandika na kufuta kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba "Tunahamia kwenye uwanja mwingine." Inaonekana hii inamfaidisha vizuri Kanye kabla hata ya kuipeleka album yake sokoni.

Mickey Drexler, CEO wa zamani wa kampuni ya GAP ameuambia mtandao wa Yahoo kwamba kampuni hiyo ya mavazi iliingiza kiasi cha ($7 million) takribani TZS. Bilioni 16.2 kwa usiku mmoja kufuatia mauzo ya Majaketi (Yeezy & Gap Jacket) ambapo uzinduzi wake ulienda sambamba na uzinduzi wa album ya DONDA, August 5 mwaka huu kwenye uwanja wa Mercedes Benz.

Jumla ya oda 35,000 zilifanyika usiku huo kwenye tovuti ya kampuni ya GAP, huku Jaketi moja likiuzwa kwa ($200) takribani TZS. 463,800

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger