.

8/25/2021

Kanye West kubadili jina, kuitwa 'Ye'

Mwanamuziki Kanye West amejaza nyaraka za kubadili rasmi jina lake kuwa Ye.
Ameeleza kuwa na ''sababu zake binafsi'' katika nyaraka za mahakama zilizowasilishwa huko Los Angeles.

Hatua hiyo inakuja miaka mitatu baada ya nyota huyo wa muziki, mwanamitindo na aliyekuwa na ndoto za kuwania urais wa Marekani kuandika katika ukurasa wake wa twitter kuhusu kubadili jina lake, baada ya kutoa albamu yenye jina Ye.

Ye inawakilisha ufupisho wa jina lake la sasa, mwanamuziki huyo mwenye miaka 44 awali alisema jina jipya kwake lina umuhimu mkubwa katika dini.

''Ninaamini 'ye' ni jina lililozoeleka kutumika kwenye Biblia, na kwenye Biblia ina maana 'You' ''West alisema mwaka 2018, alipokuwa akizungumzia albabu yake akiwa na mtangazaji wa redio Big Boy.

''Hivyo mimi ni wewe, mimi ni sisi, ni sisi. Ilianzia kwa Kanye , linalomaanisha pekee na kuwa Ye- ikiangazia uzuri wetu, ubaya wetu, kuchanganyikiwa kwetu, kila kitu.''

Nyota huyo anatarajiwa kutoa albamu nyingine, kwa jina la mama yake Donda, ingawa kutolewa kwa albamu hiyo kumekuwa kukiahirishwa mara kadahaa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger