'Wanaorudishwa Kazini si wa vyeti Feki’ Ufafanuzi Watolewa na SerikaliSERIKALI imefafanua kuhusu agizo la hivi karibuni la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kurudishwa watumishi kazini na kusema walengwa si waliokutwa na vyeti feki, bali walioondolewa kimakosa.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (pichani) alitoa ufafanuzi huo jana kwa waandishi akisema wiki hii kumetokea hali ya sintofahamu baada ya mtumiaji wa mitandao mmoja kueneza habari kuwa Waziri Mkuu ametangaza kuwa watumishi walioondolewa kazini kutokana na kukutwa na vyeti feki, wamerudishwa kazi.

“Taarifa hii ni ya upotoshaji. Alichokisema Waziri Mkuu ni kuwa watumishi 4,380 waliorudishwa kazini ni wale walioondolewa kimakosa mwaka 2017. Na hawa ni wale watumishi ambao waliajiriwa kabla ya mwaka 2004 wakiwa na sifa ya darasa la saba,” alisema Msigwa.

Alifafanua kwamba, Majaliwa aliagiza wakurugenzi wa halmashauri kuwasilisha orodha ya watumishi ambao wana sifa ya kurudishwa ili wafanyiwe kazi.


Msigwa alisisitiza: “Kwa hiyo si kweli kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu kaagiza watumishi walioondolewa kwa vyeti feki warudishwe kazini kama inavyoenezwa.”

Katika hatua nyingine: Msigwa ametambulisha mwogozo wa uendeshaji wa akaunti za mitandao ya kijamii ya serikali.

“Kama mnavyojua mitandao ya kijamii imekuwa sehemu muhimu ya mawasiliano. Kwa kutambua hilo, Idara


ya Huduma za Habari (MAELEZO) tumeandaa mwongozo wa jinsi akaunti za mitandao ya kijamii za serikali zitakavyoendeshwa,” alisema.

Aliomba maofisa na Viongozi wa Serikali wanaoendesha mitandao ya kijamii ya Wizara, Idara, Taasisi, Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuzingatia mwongozo huu ambao lengo lake ni kuhakikisha utoaji taarifa za serikali kupitia mitandao ya kijamii unazingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali

ya utoaji taarifa badala ya kila ofisa kufanya atakavyo.

Alisisitiza: “Tunataka kuepusha kuweka maudhui yasiyofaa katika akaunti rasmi za Serikali. Pamoja na mwongozo huu, Serikali inaendelea kuhakikisha akaunti rasmi zote zinathibitishwa ili ziweze kuaminiwa.”


Alitoa mwito kwa maofisa habari wote wa serikali na viongozi kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kuwa ni njia muhimu ya kuwasiliana na wananchi.

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

💥NAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

💥NAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad