.

8/18/2021

Kesi ya IDRIS Sultan ya Makosa ya Kimtandao Yafutwa

 


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeifuta kesi ya upandishaji wa maudhui mitandaoni bila kibali, iliyokuwa ikiwakabili muigizaji Idris Rashid Sultan, pamoja na meneja wake Docta Ibrahim Ulimwengu na mchekeshaji Isihaka Hassan Mwinyimvua (Wong Lee).

Kesi hiyo iliyosikilizwa mbele ya hakimu Lubologa imefutwa kufuatia uamuzi wa mkurugenzi wa mashitaka (DPP) wa kutoendelea na kesi hiyo uliotolewa kwenye barua iliyotumwa mahakamani Kisutu leo tarehe 17 Agosti, 2021.

Tarehe 18, Machi mwaka 2020, Idris Sultan pamoja na wenzake wawili walifikishwa mbele ya mahakama ya Kisutu kwa kosa la kupandisha maudhui bila kibali kwenye mtandao wa kijamii wa YouTube.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger