.

8/06/2021

Kesi ya Mbowe na Wenzake Yaahirishwa hadi 13 Agosti 2021Kesi ya ugaidi inayomkabili  Freeman Mbowe na wenzake 3 katika Mahakama ya Kisutu imeahirishwa hadi 13 Agosti 2021, baada ya upande wa Serikali kudai taratibu za kuifungua kesi hiyo katika Mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza kutokamlika.
Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo  leo Ijumaa, Agosti 6, 2021  asubuhi wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger