.

8/16/2021

Kiongozi wa upinzani aliyejaribu kuwania urais kwa miaka 15 atarajia ushindi

Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema anatarajiwa kupata ushindi wa uchaguzi wa urais wa Zambia, ambapo rais aliyepo madarakani Edgar Lungu ametangaza kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki wakati kura zikiendelea kuhesabiwa.
Katika vituo vya kupigia kura 62 kati ya 156 nchini Zambia,, Hichilema ana kura 63% dhidi ya Lungu akiwa na 35%.

Wakati matokeo yakiwa yanajieleza wazi, Hichilema anaonekana kupata ushindi wa kishindo kutokana na rekodi ya watu waliojitokeza kupiga kura.

Na yeyote atakayeshinda anahitajika haraka kuimarisha uchumi wa Zambia, jambo ambalo limekuwa kitovu cha kampeni za uchaguzi.

Kuweza kufanikiwa kukabiliana kwa haraka na madeni ya muda mrefu ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa itakuwa jambo muhimu, kama watakavyomaliza mazungumzo ya urekebishaji na wadai wa kigeni.

Zambia inakuwa taifa la kwanza barani Afrika, wakati huu wa mlipuko -kushindwa kulipa deni mwezi Novemba wakati ambao itaacha kulipa riba kwa kutumia mikopo mingine.

Lungu, ambaye aliingia madarakani mwaka 2015, alisema Agosti 12, kuwa uchaguzi ulichafuliwa kwa sababu ya vurugu katika majimbo matatu ambapo Hichilema alifanya vizuri zaidi.

Lakini waangalizi wa Umoja wa Ulaya walisema siku ya Jumamosi kuwa kulikuwa na upendeleo kwa Lungu wakati wa kampeni, rasilimali za taifa hilo zilitumiwa vibaya na vyombo vya habari vilimpendelea kiongozi aliyepo madarakani.

Hata hivyo chama cha Hichilema-United Party for National Development kilipuuzia madai ya Lungu.

"Upande mwingine wanajua wazi kuwa wameshindwa na wanajaribu kuvuruga uchaguzi wote ili kuokoa kazi zao,"msemaji Anthony Bwalya alisema.

"Wameshakata tamaa kuwa huu ndio mwisho wao wa kuwa madarakani."

Lungu, 64, alisema chama chake kinafikiria kuchukua hatua nyingine.

Washindi wanapaswa kupata ushindi wa zaidi ya nusu ya kura ili kuzuia uchaguzi kurudiwa.

Kisheria atakayeshindwa katika matokeo anaweza kutuma maomba kwa mahakama ya katiba ndani ya siku saba, hivyo kutakuwa na wiki mbili ya kusikiliza kesi.

Rekodi ya Kidemokrasia

Hichilema, anayejulikana kama HH, ana shahada ya uchumi pamoja na MBA kutoka chuo kikuu cha Birmingham nchini Uingereza.

Ana miaka 59-ni mfanyabiashara katika kilimo na utalii, aliwahi kujaribu kuwania urais wa nchi hiyo kwa mara tano na kushindwa.

Je atashinda urais?

Mipango ya Hichilema ni kulipa deni la IMF mapema awezavyo na kuanzisha mazungumzo ya kitaaluma juu ya ulipaji wa madeni.

Barani Afrika ,Zambia bado inaonekana kuwa na demokrasia baada ya kuwa na mabadiliko ya serikali mara mbili tangu utawala wa hayati Kenneth Kaunda uishe mwaka 1991.

Chama cha Patriotic Front kiliingia madarakani mwaka 2011 chini ya uongozi wa Michael Sata na Lungu alichaguliwa mwaka 2015 baada ya kifo cha Sata wakati yupo madarakani.

Ofisi ya ubalozi wa Marekani mjini Lusaka, ilitoa angalizo kuwa Marekani inaweza kuweka vikwazo iwapo mtu yeyote atahamasisha ghasia , rushwa na kukiuka haki za demokrasia wakati wa uchaguzi huru.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger