.

8/29/2021

Liverpool yabanwa mbavu dhidi ya Chelsea pungufuWENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.

Chelsea ilimaliza pungufu leo baada ya Reece James kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei kwa kuunawa mpira kwenye boksi na kusababisha penalti ambayo Mohamed Salah aliifungia Liverpool.

James aliikutwa na majanga hayo baada ya kuisaidia Chelsea kupata bao la kuongoza dakika ya 22 kwa kazi yake nzuri kumaliziwa na mfungaji Kai Havertz na sare hiyo inafanya timu zote zifikishe pointi saba baada ya mechi tatu za mwanzo.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger