.

8/16/2021

Mama Mzazi wa Romy Jons Afunguka Alipo Baba Mzazi Rommy "Aliangua Chooni"
Leo ni Birthday ya Dj maarufu nchini na East Afrika kiujumla @romyjons lakini pia ni kaka wa mwanamuziki nguli Afrika @diamondplatnumz .Ikiwa anaadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa, Mama mzazi wa Rommy ametujuza kuhusu Baba yake mzazi wapi alipo maana hatujawahi mjua.

Mama Rommy akifunguka kwenye waves za @wasafifm amedai walimzaa Rommy kabla ya kuoana,walikuja oana Rommy akiwa na umri wa miaka miwili na baadae baba mzazi wa Dj huyo alisafiri kwenda Italy ambapo bahati mbaya alipatwa na matatizo, mawasiliano yalikuwepo baina yao ila baada kama ya siku mbili toka kuwasiliana kwao alipata taarifa kuwa bwana wake amedondoka chooni na kufariki dunia.

Mwili ulirudi baada ya siku 28,hivyo Mama mzazi wa Rommy ilimbidi kurudi nyumbani kwao kumlea Rommy huku akihangaika kwenye mihangaiko yake kumsomesha mwanae na mara nyingi alimuacha kwa mama mzazi wa Diamond kila alipokuwa akienda kwenye mizunguko yake ya biashara.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger