.

8/31/2021

Marekani yaharibu ndege na vifaa vyake vya kijeshi walivyoviacha Afghanistan

Jeshi la Marekani lilihakikisha linalemaza ndege zao na magari ya silaha waliyoyaacha kwenye uwanja wa ndege mjini Kabul kabla ya kuondoka usiku wa Jumatatu. Maafisa wameeleza.
Kamanda wa majeshi ya Marekani Jeneralo Kenneth McKenzie amesema vikosi ''vililemaza'' ndege zake 73, na magari 70 ya silaha na magari mengine ya kijeshi ili Taliban wasiweze kuyatumia.

''Ndege hizo hazitaweza kuruka tena.....Hakuna mtu yeyote atakayeweza kuyaendesha,'' alisema.

Video iliyotumwa na mwandishi wa habari wa Los Angeles imes ilionesha Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege eneo ambalo ndege za Marekani zimeegeshwa wakionekana kukagua vifaa hivyo.

Pia Marekani imelemaza mfumo wa roketi wa teknolojia ya juu-ulioachwa uwanja wa ndege. Mfumo wa C-RAM ulifanya kazi Jumatatu kudhibiti shambulio la roketi la wanamgambo wa IS lililolenga uwanja wa ndege.

Kama tulivyoripoti awali, wapiganaji wa Taliban katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita wameonekana wakiwa na vifaa vya kijeshi vya Marekani na vyombo vya moto. Vifaa hivyo vilikuwa vimegawiwa kwa jeshi la Afghanistan, lakini baada ya jeshi la Afghanistan kuweka silaha chini, vifaa hivyo viliingia mikononi mwa Taliban.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger