google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mbowe Amgeuzia Kibao DPP | UDAKU SPECIAL

Mbowe Amgeuzia Kibao DPP

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kukubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mda huu amefikishwa katika Mahakama kuu kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo.

 

Katika shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linalosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya lilipangwa kutajwa leo Agosti 30, 2021.

 

Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kosa la ugaidi kupelekwa mahakamani kimyakimya bila kumtaarifu wakili wake.

 

Sambamba na madai hayo ya anadai haki zake kukiukwa kwa kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilisha kuwajulisha ndugu zake na wakili wake, pia Mbowe anadai kuwa wakati alipokwa ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa afisa wa polisi.

 

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyoungianishwa na washtakiwa wengine waliokuwawameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad