Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa Akwepa Mtego wa Polisi


Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa ameingia Bungeni Majira ya saa Moja Asubuhi kutii wito wa kwenda mbele ya kamati ya Bunge ya haki Maadili na madaraka ya Bunge akiwa peke yake bila kusindikizwa na Polisi.

Siku ya Jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliomba kibali cha kukamatwa kwa Mbunge huyo ili kufikishwa mbele ya kamati kutokana na kukaidi kufika katika siku aliyopangiwa.

Baada ya kufika Bungeni Jerry alielekea Jengo la Utawala na baadae ilipofika Majira ya saa Nne akaingia kwenye Ukumbi wa kamati ya Maadili kabla ya Mwenyekiti na wajumbe wake kuingia.

Alipoingia mwenyekiti wa kamati hiyo Emanuel Mwakasaka akaamuru mbunge huyo atoke nje ya Ukumbi na Asubiri kuitwa kama utaratibu unavyosema.

đź’ĄNAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SERIKALINI

đź’ĄNAFASI ZA AJIRA ZILIZOTANGAZWA LEO SEKTA BINAFSI

đź’ĄNAFASI ZA INTERSHIP MAKAMPUNI MBALI MBALI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad