.

8/17/2021

Mbwana Samatta Aonywa, Avuliwa number ya Jezi na Ozil, Apewa Namba Isiyo na Bahati Fenerbahce


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ameonywa mapema huko Uturuki huku akitakiwa kufanya kazi ya ziada msimu huu wa Ligi Kuu nchini humo, Supa Ligi 2021/22 ili yasijekumkuta ya mwenzake, Henri Bienvenu.

Bienvenu ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa la Cameroon, aliyewahi kuichezea Fenerbahce kwa miaka miwili huku awamu yake ya mwisho akiitumia jezi nambari 15 ambayo msimu huu kwenye chama hilo inavaliwa na Samatta.

Kwa mujibu wa Butterball Tom ambaye ni mdau wa michezo Uturuki, alisema, “Ni kweli jezi namba 15 sio ya bahati kwa Fenerbahce, lakini hilo haliwezi kumfanya Samatta ashindwe kufanya vizuri, anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kufanya makubwa na namba hiyo, anatakiwa kujituma zaidi msimu huu.”

Kwa Samatta jezi namba 15 ana historia nayo nzuri kwani wakati akiwa TP Mazembe aliwahi kuivaa na kufanya makubwa, lakini jambo hilo ni tofauti kwa Bienvenu hakuwa na bahati na namba hiyo na ndio maana baada ya kurejea kwenye klabu hiyo akitokea Real Zaragoza alipokuwa akicheza kwa mkopo mambo yalimwendea kombo.


Na inaelezwa hata kabla ya Bienvenu kuvaa namba hiyo ndani ya msimu wake wa mwisho, Fenerbahce 2012/13 aliyemtangulia, Volkan Babacan ambaye alikuwa kipa naye hakuwa na bahati na namba hiyo, aliishia kusota benchi kabla ya kutimka.

Baada ya Bienvenu kuondoka wapo wachezaji kadhaa ambao waliendelea kuitumia namba hiyo, akiwemo kiungo, Uygar Zeybek na beki wa kati, Serdar Aziz na hakuna kati yao ambaye mambo yalimnyookea.

Zeybek aliishia kucheza michezo miwili tu tena kwa dakika nne, walau mwenzake Aziz alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara moja moja lakini baadaye ilimbidi kubadili namba hiyo na sasa anatumia, namba nne na tayari umri umemtupa mkono.


Aziz alipoitema jezi namba 15 ndipo alipoichukua kipa, Harun Tekin ambaye ni chaguo la pili, kipa namba moja Fenerbahce ni Altay Bayindir.

Samatta amechukua jezi hiyo, kwa Tekin ambaye ni chuguo la pili na hadi sasa nahodha huyo wa Taifa Stars kwenye michezo saba ya kirafiki amefunga bao moja.

Awali, Samatta alikuwa akivalia jezi namba 10 ambayo imebidi amwachie supastaa Mesut Ozil.

Ozil ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki, alijiunga na Fenerbahce akitokea Arsenal ambako katika siku zake za mwishoni hakuwa akipata nafasi ya kucheza.


Umaarufu mkubwa wa Ozil, ambaye pia ni rafiki wa rais wa taifa la Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, umemfanya staa huyo kumvua Samatta jezi Namba 10 katika kikosi cha Fenerbahce.

Samatta alikuwa akivaa jezi Namba 10 alipokuwa katika klabu aliyong’aa ya Genk ya Ubelgiji na alipohamia Aston Villa ya England, alivaa jezi Namba 20.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger