.

8/19/2021

Millard Ayo Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Ajali ya Gari ya Wafanyakazi Wake iliyochukua Uhai wa Wawili


Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team…. tumeondokewa na Marafiki zetu wawili na mmoja ni Mfanyakazi mwenzetu Mpiga picha wa AyoTV Kanda ya Ziwa Nellyson Grigery (alievaa shati la kijani) na mwingine ni Rafiki yetu Mujitaba Yusuf (hayupo kwenye picha) waliekua wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar, wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu Mtu tatu ambae ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa @dullahtza (alievaa t-shirt nyekundu) amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri.

Daima tutawakumbuka Ndugu zetu hawa, daima tutamkumbuka Nellyson kama Kijana Mchapakazi, humble sana, mwenye kujituma na mwenye nidhamu kubwa sana ya kazi na hata nje ya kazi….. A VERY SAD DAY yani, Nelly alianza kazi hapa TZA (AyoTV) miezi michache tu iliyopita lakini alileta utofauti mkubwa na mchango wake unaonekana, kazi yake ya mwisho kuchukua picha za video ilikua ni interview ya Mtoto wa miaka 9 anaemsaidia Bibi yake Mgonjwa ambayo niliipost juzi…. #RIPNelly #PumzikaMkaliwetu #RIPMujitaba Tutaonana baadae Watu wangu ๐Ÿ™๐Ÿฟ
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger