.

8/25/2021

Mtangazaji Aachwa Baada ya Kulipa Mahari


MTANGAZAJI wa chombo cha habari cha Citizen cha Kenya Trevor Ombija ameeleza masikitiko yake baada ya kuachwa na mpenzi wake mnamo Agosti 23 mwaka huu.

Trevor alikiri kuumizwa sana na kitendo cha mpenzi wake huyo kumbwaga baada ya yeye kumlipia mahari na alijaribu kila njia kuokoa penzi lao lakini ilishindikana.


Inaelezwa kuwa Trevor na mpenzi wake huyo walidumu kwenye mahusiano kwa miaka 10 na katika mwaka wa sita tangu waingie kwenye mahusiano, aliamua kuachana na ukapera na kulipa mahari lakini mpenzi wake aliondoka ghafla kwa madai ya kutaka kujitambua zaidi.

Trevor amesema, “Niliumizwa sana, nipo single na sitafuti mpenzi kwa sababu bado sinapona majeraha, usiingie kwenye mahusiano ukiwa bado na maumivu”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger