.

8/27/2021

Mwalimu Mkuu aliyemkaribisha Amber Rutty aonywaHalmashauri ya Manispaa ya Temeke imempa onyo Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nzasa iliyopo Temeke kwa kutembelewa na msanii Amber Rutty akiwa amevaa mavazi kinyume na maadili ya Tanzania

Taarifa hiyo imetolewa kwenye barua waliyoichapisha Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwenda kwa vyombo vya habari kuhusu kukanusha ugeni huo katika shule hiyo.

Barua hiyo inaeleza kwamba "Kumekuwa na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video clip kinachozunguka katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha mtu mmoja akitembelea shule ya msingi Nzasa akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania" 

"Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo pia hauhusiki kwa namna yoyote juu ya mualiko wa mgeni huyo"

"Aidha uongozi wa Manispaa ya Temeke umemuonya Mkuu wa shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea, uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wote uliojitokeza"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger