Mwanafunzi kidato cha nne abuni kifaa cha kukusanya mapato

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Ufundi ya Iyunga ya Mkoani Mbeya,Yusuph Ng’umbi amebuni kifaa kiitwacho Public Area  Accounter ambacho kitasaidia kukusanya mapato katika maeneo ya wazi yenye shughuli za kijamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Agosti 20,2021, waliofika shuleni hapo kuangalia ubunifu unaofanywa na wanafunzi wa shule hiyo, mwanafunzi huyo amesema  kifaa wamekitengeneza ili kiwe na uwezo wa kusimamia sehemu ambazo kuna ukusanyaji wa fedha.



Mfumo wetu tumeutengeneza kwa sababu sio wote ambao wanakusanya mapato ni waaminifu baadhi yao huwa wanachukua kiasi cha hela na kupunguza mapato katika serikali.
“Sasa huu mfumo wetu tumeutengeneza ambapo mkusanyaji akiishakusanya hela mtu akipita katika hilo eneo atahesabiwa na kuonekana mtu mmoja amepita na itahesabu hela aliyotoa.

ALIPOLIPATA WAZO

Mwanafunzi huyo amesema wazo hilo alilipata wakati akiwa kituo cha basi na rafiki zake ambapo walianza kubishana kwamba fedha ambazo zimekuwa zikikusanywa katika vyoo vya kulipia hazifiki katika Halmashauri zote kwani baadhi wamekuwa wakijinufaisha.

“Wazo hilo lilikuja kipindi cha Corona nilikuwa na marafiki zangu tukiwa kituo cha basi tukawa tunabishana  kuhusiana na vyoo vya kulipia tukajadiliana kwamba jamaa hapeleki hela kamili katika Halmashauri kwahiyo tuliporudi mwezi wa sita tukaanza kulifanyia kazi,”amesema

ATUMIA MIEZI SITA KUTENGENEZA

Amesema ametumia miezi sita kukamilisha Project hiyo ambapo walipofika wataalamu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia waliipeleka katika Mashindano ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) Mkoani Dodoma.

 “Huu mfumo tumeutengeneza uwe unakaa sehemu uliyojificha hata msimamizi hawezi kujua na hawezi kujua sehemu gani umekaa na tumeweka mfumo huu  mtu asiweze kuingilia na kuuchezea,”amesema

WAISHUKURU WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA



Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Iyunga Edward Mwantimwa ametoa shukrani kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuwaendeleza wabunifu katika shule za Sekondari.
Amesema shule hiyo  imekuwa ikitoa wanafunzi wenye vipaji ikiwemo mwanafunzi aliyebuni kifaa cha kukusanya mapato katika Halmashauri



“Wanafunzi wamefanya ubunifu kupata uhalisia wa mapato kama kiingilio madhalani katika Standi,sokoni akitaka kujua wanachaji shilingi ngapi  anamweka mtu kutokana na uaminifu wake, mfumo huu unaweza kutatua changamoto.
“Pia jinsi gani rahisi ya kuweza kupata uhalisia wa mapato yanayopatikana katika kuchaji hasa katika kiingilio madhalani Sokoni anataka kujua anachaji shilingi ngapi lakini anamweka mtu ambaye inategemea uaminifu wake,” amesema

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad