.

8/30/2021

Mwanamke mmoja afariki 'baada ya kupata chanjo ya Pfizer' New Zealand

New Zealand imeripoti kile inachoamini kuwa kifo cha kwanza kinachohusisha chanjo ya corona ya Pfizer.
Bodi huru inayoangazia usalama wa chanjo nchini humo imesema kifo cha mwanamke huyo ''pengine'' ni kutokana na maumivu ya misuli ya moyo.

Pia imesema kulikuwa na changamoto nyingine ambazo kuna uwezekano zilisukuma athari za chanjo kutokea.

Waangalizi wa Ulaya wamesema kuwa ugonjwa huo ni ''nadra'' na kuwa faia ya chanjo ni kubwa zaidi kuliko athari maya za chanjo.

Taarifa rasmi kuhusu sababu ya kifo bado haijatolewa.

Hatahivyo, Bodi inayoshughulikia usalama wa chanjo ya Covid-19 imesema kuwa maumivu ya misuli ya moyo ''pengine yalitokana na chanjo''.

"Hii ni kesi ya kwanza huko New Zealand ambapo kifo kimehusishwa na chanjo ya Pfizer COVID-19. Wakati Kituo cha Ufuatiliaji wa athari mbaya kimepokea ripoti nyingine za vifo kwa mtu aliyepewa chanjo ya hivi karibuni, lakini hakuna taarifa ya kifo inayohushwa na chanjo, "kilisema katika taarifa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger