.

8/07/2021

Nandy Siri Yake ya Ghana Yafichuka

WIKI iliyopita sexy lady kwenye tasnia ya Bongo Fleva, Faustina Charles au Nandy alisafiri kuelekea nchini Ghana ambapo safari hiyo iliibua maswali mengi, lakini mwenyewe amefichua kilichompeleka huko.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Nandy anasema kuwa, alikwenda nchini Ghana kwa kazi ya kimuziki kwa mwaliko wa msanii Mr Eazi.

 

Kwa mujibu wa Nandy, alikwenda Ghana kurekodi ngoma mpya ambapo aliambatana na prodyuza wake aitwaye Kimambo.Nandy anasema kuwa, yupo kwenye harakati za kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa Afrika. Awali, Nandy alitangaza kuwa, alikuwa studio na msanii wa Afrika Kusini, Sho Madjozi kwa sababu ya kurekodi kolabo yao.

 

Nandy anaongeza kuwa, mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani amefanya kazi nyingi za kimataifa.Kwa sasa, Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wanaofanya poa kinoma ndani na nje ya Bongo.

 

Nandy anafahamika kwa tamasha lake la Nandy Festival ambalo limevutia watu wengi huku akimshusha Joe Boy wa Nigeria na kutumbuiza mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger