.

8/16/2021

Nandy "Bei ya Gari Yangu ni Kubwa sana Sawa Ukitumia Laki moja Kwa Siku Kwa Miaka 60"
Muimbaji wa Bongo Flava @officialnandy amedai hawezi taja bei ya gari lake aina ya Range Rover Evoque ni kiasi gani ila ni pesa ndefu sana.

Nandy amefunguka kuwa kiasi cha pesa alichotumia kununulia mkoko wake kama angeamua kutumia laki moja kwa siku basi ingemchukua zaidi ya miaka 60 kumaliza pesa hiyo. Hii ina maana kuwa mkwanja uliotumika kuchukua huo mkoko ni mrefu kichizi.

Range Rover Evoque 2021 inaanzia dolla za kimarekani $43,300 na bei ya juu zaidi ni $53,400 ila inaweza kugharimu hadi $71,000 (zaidi ya Tsh 164M ) ikiwa utataka kuongezea baadhi ya vitu. Na hii ni bei nje na mambo ya ushuru na leseni gari ikitua nchini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger