.

8/18/2021

"Penzi Letu sio la Kwanza Kuisha" - Billnass

 


Kupitia page ya Instagram anayotumia rapa Billnass siku za hivi karibuni ameshea picha mbili na video moja akiwa amemshika mtoto ambaye amem-tag kwa jina la Nenga Tronix.

Kulia ni picha ya Billnass akishika mtoto, kushoto ni Nandy

Watu wengi wameuliza kuhusu mtoto huyo na  wengine wakitaka kujua mama wa mtoto huyo, na vipi hatma yake na Nandy ambao stori zinasemekana wametemana kwa sasa.

Sasa leo kupitia Insta story yake amezua gumzo kwa kupost ujumbe unaotafsirika kama hali si shwari kwenye mahusiano yake na Nandy baada ya kuandika.

"Penzi letu sisi sio la kwanza kuisha, ugomvi wetu yeye hajui chanzo wala kisa yeye ni malaika usimuweke kwenye vita" 

Wawili hao yalijulikana wazi kuanzia mwaka 2018 na miaka miwili baadaye 2020 walichumbiana na kuahidi mipango ya ndoa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger