.

8/24/2021

Profesa Jay Ageukia Utangazaji


Mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo ambaye pia ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mikumi kwa leseni ya Chadema, Joseph Haule almaarufu Profesa Jay ameamua kugeukia kwenye utangazaji.

 

Profesa Jay ametambulishwa jana, Agosti 23, 2021 kuwa ni miongoni mwa usajili mpya wa Kituo cha Redio cha Clouds FM ambapo atasikika kwenye kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast akiwa na Masoud Kipanya na Barbara Hassan.

 

Habari za ndani zinadai kwamba, Profesa Jay ameziba pengo lililoachwa na mtangazaji Fred Fidelis almaarufu Fredwaa ambaye alifariki dunia Juni 12, 2021 kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Kawe jijini Dar.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger