.

8/16/2021

Rais Mstaafu Trump amtaka Rais Biden ajiuzuluRais wa zamani wa Marekani Donald Trump amemtaka Rais wa sasa Joe Biden ajiuzulu akimtuhumu kusababisha Wanamgambo wa Taliban kupata nafasi ya kutawala Miji mbalimbali ya Afghanistan ikiwemo Mji Mkuu wa Kabul, hii ikiwa ni baada ya uamuzi wake kuliondoa Jeshi la Marekani nchini humo lililokaa kwa miaka takribani 20.
“Ni wakati umefika sasa kwa Joe Biden kujiuzulu kwa kile alichokisababisha kwa Watu wa Afghanistan na wala haitokuwa jambo kubwa maana hakuteuliwa kihalali tangu mwanzo, Biden ameshindwa pia kuidhibiti Corona, kupambana na masuala ya Uchumi na Wahamiaji” Trump

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ameikimbia Nchi yake ya Afghanistan jana baada ya Wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa Kabul.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger