.

8/09/2021

Rais Samia Ahojiwa Kuhusu Mashtaka ya Mbowe
RAIS wa Samia Suluhu Hassan amesema hawezi kuzungumzia kesi ya kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi.


Kwa mujibu wa BBC, katika mahojiano maalum na mwandishi wa BBC, Salim Kikeke, Rais Samia amesema Mashtaka dhidi ya Mbowe hayajachochewa kisiasa, ana imani sheria itachukua mkondo wake.

Wafuasi wa Mbowe wanadai kuwa mashtaka haya yamechochewa kisiasa. Aidha, katika suala la demokrasia na uhuru wa kujieleza Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu wana uhuru wa kutosha. Mahojiano hayo yatarushwa leo Jumatatu, kupitia Dira ya Dunia ya BBC.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger