Ripoti kuhusu afisa wa polisi Nigeria kuwa na ushirika na tapeli wa mitandaoni Hushpuppi yatolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




Mkuu wa polisi wa Nigeria amepokea ripoti ya uchunguzi kuhusu afisa wa juu aliyesimamishwa kazi Abba Kyari, ambaye anatafutwa kwa madai ya kuwa na ushirikiano na tapeli wa mtandao wa Instagram Hushpuppi.



Bw Kyari alisimamishwa kazi kama naibu kamishna wa polisi kufuatia kushtakiwa kwake na mamlaka ya Marekani kwa madai kwamba aliwezesha malipo kwa wafanyakazi wa polisi wa Nigeria kutoka kwa Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas.

Hushpuppi
Hushpuppi/Instagram Copyright: Hushpuppi/Instagram
Polisi wa Nigeria waliunda jopo la kufanya ukaguzi wa ndani wa madai hayo baada ya mashtaka ya Marekani Bw Kyari anakanusha madai hayo yote.

Siku ya Alhamisi, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Joseph Egbunike aliwasilisha ripoti ya jopo hilo kwa mkuu wa polisi Usman Baba, bila kufichua maelezo ya matokeo yao.

Bwana Egbunike alisema ripoti hiyo ni matokeo “ya mchakato wa uchunguzi wenye bidii, wazi na kamili”. Mkuu wa polisi alitaja kujitolea kwake kwa haki na akasema timu ya usimamizi wa polisi itapitia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa “hatua muhimu”.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad