.

8/26/2021

Shilole na Mmewe Hapatoshi, Shilole Hataki Aoe MKE wa Pili Adai KitaumanaMsanii wa Bongo Flava na mfanyabiashara wa chakula, @officialshilole amedai hawezi na hataki kuwa mke wa pili na pia hawezi mruhusu mumewe @rommy3d kuongeza mke wa pili.

Shishi amedai alimwambia mume wake kuwa kama akitaka mke wa pili basi achague mambo mawili, Rommy Amuache Shishi kisha aendelee na mchongo wa kubeba jiko lingine. 

Shishi amesema mke wa pili sio fashion, watu wasome dini waelewe kuna mambo mengi,uwenda mwanamke kutomridhisha mumewe na pia kuna maradhi ambayo yanaweza fanya mume kuongeza mke mwingine. Lakini pia amedai unakuta watu wanaongeza wake na nguvu za kiume hawana japo binafsi anaridhishwa na mumewe ,suala la nguvu za kiume amelisema kwa ujumla tu.

Kingine ni kuwa ukiwa unaingia Anga za Shishi ni kutafuta Mauaji ya Kimbali maana hakuna hasiyejua Shilole ni mke wa Rommy,na Rommy ni mume wa Shishi.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger