.

8/08/2021

Sihitaji kuondoka – Messi chozi lamdondoka akiwaaga Barcelona
Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi amewaaga mashabiki na viongozi wa timu hiyo huku akishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akimwaga machozi hadharani mbele ya vyombo vya habari.Chozi likimtoka, Messi kwa uchungu amesisitiza kamwe haitaji kuachana na timu hiyo kwakuwa ndiyo klabu aipendayo ”Sikuhitaji kuondoka, ni klabu niipendayo,”.Akiwa na huzuni kubwa iliyomtawala usoni mwake, Messi anahitimisha miaka 21 tangu ajiunge na miamba hiyo ya soka nchini Hispania.Ofa ya paundi milioni 25 kwa mwaka linamsubiri Messi aanguke tu saini yake, ambapo ni dili la miaka miwili kujiunga na matajiri wa Ufaransa Paris Saint-Germain ambao wanaonekana kuwa wamoto kweli kweli wakiwa tayari wana beki bora na mwenye viwango vya Dunia, Sergio Ramos wakati huo huo wakiwa na Neymar pamoja na Kylian Mbappe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger