.

8/25/2021

Silaa atoa ujumbe kwa wabunge, kuhojiwa tena Alhamisi
Dodoma. Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ametakiwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kurejea tena katika kamati hiyo siku ya Alhamisi Agosti 26 2021 kuendelea na shauri lake la kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Agosti 21 mwaka huu, Ndugai aliagiza Silaa na Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima wahojiwe na kamati hiyo kwa tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Akizungumza baada ya mahojiano hayo leo Jumanne Agosti 23, 2021 Mwenyekiti wa kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema kuna mambo machache yaliyobakia ambayo watafanya naye tena mahojiano Alhamisi Agosti 26 2021.

Kwa upande wake katika viwanja vya Bunge, Silaa amesema wabunge wakati wote wanapotekeleza majukumu yao wanalo jukumu kubwa la kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kuwa Serikali inafanikiwa.


 
Amesema kuwa yeye atahakikisha kuwa kazi hiyo anaifanya wakati wote.

Soma zaidi: Silaa agoma kusindikizwa na askari

“Tujitahidi sana tutekeleze matakwa ya Katiba kifungu cha 63 ibara 8:1 ya kuweka maslahi ya wananchi mbele,”amesema Silaa.


Amesema wakumbuke katika mamlaka yote ya kibinadamu yako mamlaka makubwa ya juu ya Mwenyezi Mungu.

Amesema katika kazi zao zote wabunge wanatakiwa kumtangulize Mungu na wasitengeneze mazingira mengine ya kibinadamu.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger