.

8/17/2021

Simba na Kagera sugar Hapatoshi Sakata La Mchezaji Yusuph MhiluAnaandika Alikamwe kuhusu sakata la Kagera sugar na klabu ya Simba sc.

"Imebainika kuwa Simba sc ilimtambulisha Yusuph Mhilu bila kumalizana na Uongozi wa Kagera sugar... Mhilu bao anamkataba wa mwaka mmoja na Kagera sugar"

"Baada ya Simba kumtambulisha bila makubaliano na klabu ya Kagera sugar, Kagera wametaka Tsh 200 Milioni huku Simba wakikomaa na ofa ya Tsh 35 Milioni"

"Dirisha la usajili (CAF) lilifungwa juzi, na Kagera sugar walikuwa hawajatoa 'Release letter', hivyo kama Simba watataka kumtumia Yusuph Mhilu kwenye ligi ya mabingwa Africa, watapaswa kulipa Dollars (500) kwa kuchelewesha kutuma jina"

"Kwenye mazungumzo ya awali Simba walituma Tsh 35 Milioni lakini Kagera sugar wakaipiga chini ofa hiyo wakitaka Tsh 50 Milioni ili wamtoe Mhilu"

"Wakati Mazungumzo hayo yakiendelea, Simba wakamtambulisha Yusuph Mhilu, kitendo kilichowakwaza viongozi wa Kagera sugar wakahisi KUDHARAULIWA"

"Baadae kiongozi mmoja wa Simba aliwaomba radhi Kagera sugar kuwa utambulisho ule ulifanywa kimakosa na mtu mmoja wa idara ya habari. Hivyo wakawaomba wasikanushe chochote huku mazungumzo yakiendelea"

"Lakini Kagera sugar wakashtuka baada ya kuitwa (TFF) kuwa wamefunguliwa mashitaka na Yusuph Mhilu akitaka kuvunja mkataba"

"Baada ya kesi kusikilizwa na kuonekana Kagera wanahaki na mhilu anatakiwa kufuata vizuri taratibu za klabu ili kuvunja mkataba,, Uongozi wa Kagera sugar sasa umepanga kuishitaki Simba kwa kumtambulisha Mchezaji wao na kuhitaji kiasi cha Tsh 200 Milioni ili wamruhusu"

๐Ÿ” Ali Kamwe Mchambuzi Azam tv.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger