.

8/18/2021

Simba yamsajili Jimmyson Steven Mwanuke

KLABU ya Simba imemtambulisha nyota mpya mwingine mzawaeo Agosti 18 kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.

Ni Jimmyson Steven Mwanuke mwenye umri wa miaka 18 ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Gwambina FC.

Anauhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kuwa timu ya Gwambina FC ya Mwanza itashiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kushuka msimu uliopita.

Ilimaliza ikiwa nafasi ya 16 ilikusanya pointi 35 baada ya kucheza jumla ya mechi 34 anakuwa mali ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes na ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kufikisha pointi 83.

Dili la Steven ambaye ni winga inaelezwa kuwa ni miaka mitatu na atakuwa hapo mpaka msimu wa 2024.

Huyu ni nyota wa nane kutambulishwa Simba anaungana na Henock Baka, Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane, Yusuph Mhilu,Israel Patrick na Abdulsamad Kassim.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger