.

8/20/2021

Simba Yawapiga Bao WazunguWAKATI Simba SC wiki chache zilizopita ikikamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Peter Banda raia wa Malawi, imebainika kwamba, nyota huyo alikuwa na ofa kutoka Hispania na England.


Banda amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Nyasa Big Bullets ya kwao ambapo kabla ya hapo, alikuwa akicheza kwa mkopo, Sheriff Tiraspol ya Moldova.

 

Kaimu Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema: “Kwanza nitoe pongezi kwa kamati yetu ya usajili kwa kazi kubwa na yenye weledi ambayo wameifanya mpaka sasa.

 

“Kumpata mchezaji kama Banda ambaye kwao ni miongoni mwa wachezaji bora zaidi kiasi kwamba mpaka baadhi ya waandishi wa Malawi wamekuwa wakihoji, inawezekanaje Simba kumshawishi na kumsajili wakati wao wanajua alikuwa na nafasi ya kwenda Hispania au England kutokana na ofa alizokuwa nazo.

 

“Hili pia limetokea kwa kiungo mshambuliaji, Pape Ousmane Sakho ambaye kwao ndiye mchezaji bora zaidi kijana. pamoja na wachezaji wengine waliosajiliwa.

 

“Kuna watu wanauliza kwa nini tumesajili wachezaji wengi, lakini niwaambie hatujakurupuka bali tumesajili kuendana na mapendekezo ya mwalimu.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger