TANZIA: Mfanyabiashara maarufu Mtei afariki dunia

 


Mfanyabiashara maarufu mkoani Manyara, James Mtei ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya Jambo Express amefariki dunia ghafla

Awali, Mtei alikuwa mmoja kati ya wakurugenzi wa kampuni ya usafirishaji ya mabasi ya Mtei, amefariki jana Jumanne Agosti 24, 2021 akiwa nyumbani kwake.


 Elly Mtei ndugu wa marehemu amesema kaka yake amefariki ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa nyumbani kwake.


Amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwake Mrara mjini Babati.


"Baadhi ya ndugu wapo hapa mjini Babati kwa mipango ya taratibu za mazishi ili kupanga taratibu za siku na mahali maziko yatakapofanyika," amesema Mtei.


Mbunge mstaafu wa Jimbo la Babati Vijijini, Vrajilal Jituson amesema mji wa Babati na mkoa mzima wa Manyara, umepoteza mdau muhimu na maarufu wa maendeleo.


Jituson amesema wanamuombea marehemu Mtei apumzike kwa amani na jamii iige mazuri yote aliyofanya kipindi cha uhai wake.


"Alikuwa ana utu mwenye kujitoa kwa hali na mali ikiwemo usafiri na huduma za jamii, michango ya ujenzi wa shule, zahanati na maendeleo mengine, Manyara tumepata pigo kubwa," amesema Jituson.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad