.

8/07/2021

TBS imeiingizia serikali bilioni 3.9 ukaguzi wa magariWaziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo ametoa wito kwa waingizaji wa magari nje ya nchi kushirikiana ipasavyo na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika zoezi la ukaguzi wa magari bandarini yanayotoka nje ya nchi ili zoezi liweze kwenda vizuri.


Ameyasema hayo leo Agosti 5, 2021 alipotembelea bandari katika kitengo cha kukagua magari zoezi ambalo linafanywa na TBS na kujiona shughuli hiyo ikifanyika.


Katika kipindi cha mwezi Aprili hadi kufikia Agosti 3, 2021 (TBS) imekusanya takribani Shilingi Bilioni 3.9 katika zoezi la ukaguzi wa magari bandarini yanayotoka nje ya nchi na kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.7 ambayo mwanzo ilikuwa inabaki nje kabla ya zoezi hilo kuanza kufanyika hapa nchini.


Profesa kabudi awaonya watumishi wa Mahakama

Hali kadhalika mpaka kufikia Agosti 3, 2021 TBS ilifanikiwa kukagua magari 11079 na katika magari hayo 7700 yalikuwa yamekidhi ubora na magari yaliyobaki yalikwenda kutengenezwa na baada ya kutengenezwa magari 1890 yaliweza kukidhi ubora na mengine yaliyobaki yapo gereji yakiendelea kurekebishwa.


Aidha Prof.Mkumbo ametoa wito kwa waingizaji wa magari nje ya nchi kushirikiana ipasavyo na TBS ili zoezi liweze kwenda vizuri hasa kuendelea kuelezea changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza ili waweze kuzitatua.


Kwa upande wake Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa zinazotoka nje TBS, Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kuna magari 1890 hayakufahuru kwenye hatua ya awali yanahitaji marekebisho ya taa, mataili na mengineyo, na hili lote limekuwa likiwanufaisha Watanzania kwasababu yanakwenda katika gereji ambazo Watanzania wanazimiliki .


Katika utaratibu wa zamani ambapo ukaguzi wa magari kwa kiasi kikubwa ulikuwa unafanyika nje ya nchi na TBS kwa niaba ya Serikali tungepata asilimia 30% tu za fedha peke yake na asilimia 70% ingebaki nje.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

New Video - Wana Wanywe Pombe

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger